One Struggle

Verse 1
Bad friends waliniacha kwa sheol/nikaskip death kwa pot-holes/nikawa haunted nama nightmare za blackhole/ilibidi niquestion life/ i'm i living right?/nilipewa sanaa kupaint truth, na kuplant seed ya light/nipinge giza/niandike inspirational quotes, kwawenye wanataka kuskiza/before nirudi kwa land of the lost/ najituma in all cost/niandike soul yangu kwa vitabu za sasa/ akili yangu tucheze dice na salsa/nione ulimi yangu ikiperform wonders of itself/niache knowledge kwa shelf/nikumbatiye truth yenye iko uchi/sitanyamaza ata wakinishona mdomo yangu na uzi/sitaenda kinyume ya kweli kwa hii generation ya mafisi ma mbuzi/heart yangu haita-dilute positivity /niandike vitabu za revolution na creativity/hadi nibaki void,waseme kuna sauti kwa jungle imebeba change/ni elimisha marapper wanaota dream fame/dunia ni throne of games/kusurvive itabidi umebaki sober/

Hook
Tuishi one life one struggle/

Verse 2
Beba mishale ni bebe knowledge /beba vitabu twende milage/tuelimishe watoto/wajuwe kwa hii land, kuna cactus na moto/kuna cold na joto/kuhustle na ndoto/tushikane, tuchange world na sanaa/Tujenge foundation /ya new generation /watoto wetu wasipende manna,wa drink pure water from the rock,tusiwe mislead,life ni gamble/cheza kadi/tupendane tutafika mbali/kuna nyoka kwa green grass tembea makini/kuna false teachings kwa kila mu-umini/ tucheze wimbo za njiwa/one moment kwa walio-fiwa/life ni beautiful/tukiwa greatful/tufufuwe paths zilikuwa forgotten/turudishe marifa kwa hii generation iko rotten/tuwache mark kwa heart (art) na zaburi kwa tracks /natuishi one life full of truths.

Hook
Tuishi one life one struggle/

Verse 3
Mungu nipe nguvu nisipotee kwa hii kizazi,spirit inawill kustay righteous, lakini mwili imekataa/nina kula na ku-rome kwa barabara ukatili imejaa /Maafa na njaa/ubongo tuna starve/spirits tumeclash/tunakufa juu ya madini/nani wa kweli nani kafiri/najiona kasisi lakini majaribio imezidi nibariki leo kesho nduru/kilio kila dira/nikijitazama naona majonzi kwa mirror/nafsi iko dry /uwongo siwezi testify/ulinipa kipaji nibonge,so nipe one chance ni bless mic ,dunia wasipotee kwa kukosa marifa/nichambuwe methali kwa kila roho/nilete uhai ,tutoke kwa nyororo za giza/nipe one sight nione maisha ya ndani/nipe one soul nijione ndani/nikule asali ya land/nipate energy kwa mind/nataka one one nataka one struggle